Mkuu wa wilaya ya Tanganyika mh. Salehe Muhando |
TANGANYIKA
Wakulima kata ya Mpanda
ndogo wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi wameiomba serikali kupunguza gharama
za pembejeo za ruzuku.
Wakizungumza na Mpanda
redio kwa nyakati tofauti baadhi ya wakulima wamesema bei wananyonunua pembejeo
kwa sasa ni kubwa hali ambayo inawakwamisha kufikia malengo yao katika kilimo.
Wamesema serikali iweke
utaratibu ambao utawasaidia wakulima kupata pembejeo kama mbegu na mbolea
ambazo watazinunua kwa bei nafuu.
Hivi karibuni mkuu wa
wilaya ya Tanganyika DC Salehe Muhando akihojiwa na kipindi cha jioni maridhawa
kinachorushwa na Mpanda radio fm amepiga marufuku kwa mawakala wa pembejeo
kujipangia bei elekezi.
Serikali ya awamu ya
tano inayoongozwa na Rais DK John Pombe
Magufuli inahimiza Tanzania ya viwanda ilikufikia,
mpango huu mikakati inahitajika katika kuwainua wakulima nchi Tanzania
Source Rebeca
Kija
No comments:
Post a Comment