Thursday, 16 November 2017

Mkoa wa Katavi umetajwa kuwa miongoni mwa mikoa itakayo patiwa madaktari bingwa ili kurahisisha utoaji wa huduma kwa wangonjwa.


Mbunge wa viti maalumu wa CHADEMA Roda Kunchela


KATAVI

Mkoa wa Katavi umetajwa kuwa miongoni mwa mikoa itakayo patiwa madaktari bingwa ili kurahisisha utoaji wa huduma kwa wangonjwa.

Kauli hiyo imetolewa leo na Naibu waziri wizara ya Afya Dk FaustineNdugulile  alipokuwa akijibu swali la nyongeza lililo ulizwa na Mbunge wa viti maalumu wa Chama cha demokrasia na Maendeleo CHADEMA Roda Kunchela aliyetaka kujua lini serikali italimaliza tatizo hilo.

Akijibu swali hilo amesema tayari serikali imeanza kuchukua hatua za haraka kulikabili suala hilo kwa mkoa wa Katavi na maeneo mengine.

Licha ya hayo serikali ya mkoa wa Katavi iko mbioni kuanza ujenzi wa hosipitali ya rufaaa itakayo toa huduma kwa mkoa mzima.

Source: Bunge Tv

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...