Mbunge wa Mpanda vijijini Suleimani Kakoso |
DODOMA
Serikali imesema kuanzia mwaka wa
fedha 2018/2019 wanatarajia kuweka fedha katika mradi wa maji Ziwa Tanganyika ili
kuwezesha kuvuta maji kutoka Ziwa Tanganyika na kusambazwa katika maeneo
mbalimbali ya Mkoa wa Katavi.
Kauli hiyo imetolewa leo bungeni
Dodoma na Waziri wa maji na umwagiliaji Issack Kamwelwe ,wakati akijibu swali la
mbunge wa Mpanda vijijini Suleimani Kakoso aliyetaka kujua mpango wa serikali
kuvuta maji kutoka Ziwa Tanganyika hadi Mpanda Mjini.
Waziri Kamwelwe ambaye pia ni mbunge
wa jimbo la Katavi Mkoani Katavi,amesema wizara imepokea andiko la mradi huo wa kuvuta maji
kutoka ziwa Tanganyika na mradi huo utatekelezwa kama sehemu ya kumaliza tatizo
la maji Mkoani Katavi.
Kwa sasa wakazi wa Mpanda wanapata maji
kutoka vyanzo kama bwawa la milala na maji ya mseleleko Ikorongo.
source: Issack Gerald
No comments:
Post a Comment