TABORA
Kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili
baadhi ya maafisa wa benki ya posta imeendelea kuahirishwa katika mahakama ya
hakim mkazi mkoa wa tabora baada ya upande wa jamhuri kushindwa kuwasilisha
mahakamani hapo hatua ya maelezo iliyofikiwa ya upelelezi wa shauri hilo.
Mbele Ya Hakim Mkazi wa Mahakama
Tabora EMANUEL NGIGWANA Wakili Wa Serikali TITO MWAKALINGA Ameieleza Mahakama
Kuwa Anaendelea kufanya Mawasiliano na Mawakili Waliopo Kwenye Ofisi Ya
Mkurugenzi Wa Makosa Ya Jinai Nchini DPP Kuhusu Hatua iliyofikiwa ya Upelelezi
wa Jalada hilo.
Jopo La Mawakili Upande Wa
Washitakiwa Wakiongozwa Na Wakili PAULUSI RWEYONGEZA Walitaka Kujua Mahakamani
Hapo Kama Shauri Hilo Limetelekezwa Au La Kwa Kuwa Watuhumiwa Wanaendelea
Kusota Mahabusu huku wakiwa Wametenganishwa na Familia zao ambazo bado
zinaendelea kuwategemea.
Akijibu Hoja Hiyo Wakili Upande Wa
Jamhuri TITO MWAKALINGA Ameomba Mawakili Waelewe Kuwa Shauri Hilo Bado
Linafanyiwa Kazi Kisheria Na Kwamba Ofisi Ya DPP Haijawahi Kuichezea Mahakama
kama walivyokuwa Wamedai.
Kwa Upande Wake Hakim Mfawidhi Wa
Mahakama Hiyo EMANUEL NGINGWANA Amesema Kuwa Ofisi Ya DPP Itimize Majukum yake
Kisheria ili Haki Iweze Kutendeka.
Kesi Ya Uhujumu Uchumi Namba Tatu Ya
Mwaka 2017 Inayo Wakabili Watuhumiwa 16 Wakiwemo Baadhi ya Maafisa Wa Benki ya
Posta Imeahirishwa Hadi Novemba 29 Mwaka Huu Itakapo Tajwa Tena.
No comments:
Post a Comment