MPANDA
Wakulima
wa zao la tumbaku wa chama cha msingi cha ushirika Mpanda Kati Mkoani Katavi wameilaumu
serikali kushindwa kutekeleza agizo lake la kuhakikisha tumbaku iliyo kosa soko
inanunuliwa.
Wakulima hao kwa nyakati tofauti wamesema mpaka sasa hawajui hatima ya ununuzi wa tumbaku yao huku wengine wakisema wameathirika kiuchumi na maisha kwa ujumla.
Hivi
karibuni,mwenyekiti chama cha msingi cha Ushirika Mpanda Kati Bw.Sosipeter
Salvatory ,alisema kuna kiasi cha tani elfu ishirini na mbili ambazo
hazijanunuliwa kati ya kiasi chote cha tumbaku iliyozalishwa katika msimu wa
mwaka mwaka 2016/2017.
Mnamo Novemba 17 mwaka huu Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati akiahirisha vikao vya Bunge mjini Dodoma alieleza kuwepo kwa kampuni itakayo nunua Tumbaku iliyosalia pamoja na Mbaazi.
SOURCE: EATV
No comments:
Post a Comment