MPANDA.
Mtu mmoja anayefahamika kwa jina la
James Modest mkazi wa Kijiji cha Mnyaki A kata ya Katumba Wilayani Mpanda amenusurika kuuwawa baada ya watu
wanaosadikiwa kuwa majambazi kuvamia nyumbani kwake usiku wa kuamkia leo.
Kwa mjibu wa James Modest ambaye ni
Mhanga wa tukio hilo amesema ameporwa fedha taslimu shilingi laki saba,vifaa
vya sola za umeme na simu mbili kubwa na ndogo vyote vikiwa na thamani
inayokadiriwa kuwa shilingi milioni moja.
Mwenyekiti wa kijiji cha Mnyaki A
Bw. Kisele Meshack amethibitisha tukio hilo na kusema kuwa tukio hilo
limetokea usiku majira ya saa 7 usiku.
Tukio
hilo linatajwa kuwa miongoni mwa matukio manne ya kutoka katika kijiji cha
Mnyaki kata ya Katumba ambapo katika kipindi cha mwezi Januari hadi Oktoba
mwaka huu hakuna mauaji yaliyotokea bali uporaji wa mali na watu kujeruhiwa.
SORCE:Issack Gerald
No comments:
Post a Comment