Friday, 20 October 2017

UN yatoa Dola160 milioni nchini.





Mratibu mkazi wa UN, Alvaro Rodriguez
Mratibu mkazi wa UN, Alvaro Rodriguez 
Dar es Salaam. 
Umoja wa Mataifa (UN) umetoa Dola 160 milioni za Marekani kati ya Dola 200 milioni zinazitakiwa kutolewa mwaka huu kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo ikiwamo kuwahudumia wakimbizi waliopo kambi mbalimbali Kigoma.
Nusu ya fedha hizo zimeelekezwa kwenye mradi wa Kigoma wa kuwahudumia wakimbizi na kiasi kingine kimeelekezwa kwenye miradi mingine ya maendeleo inayofadhiliwa na mashirika mbalimbali ya UN.
Oktoba 24, UN itaadhimisha miaka 72 tangu kuanzishwa kwake na sherehe za maadhimisho hayo kitaifa zinatarajiwa kufanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wageni zaidi ya 500 wakiwamo na mabalozi, wanafunzi na vyombo vya ulinzi na usalama.
Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo yenye kauli mbiu ‘Maendeleo ya Viwanda na Utunzaji Mazingira kwa Maendeleo Endelevu.’
Akizungumzia maadhimisho hayo jana, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, kimataifa na kikanda, Dk Susan Kolimba alisema wameamua kuunganisha kauli mbiu ya Serikali ya kuendeleza viwanda na mpango wa UN wa kutekeleza Malengo 17 ya Maendeleo Endelevu (SDGs).
Mratibu mkazi wa UN, Alvaro Rodriguez alisema programu ya Kigoma imebuniwa ili kukidhi vipaumbele vya maendeleo ya mkoa huo na hasa kuzilenga jamii katika wilaya za Kasulu, Kibondo na Kakonko.
@habari na mwananchi

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...