Monday, 23 October 2017

Rais awatunuku vyeti wajumbe wa kamati za makinikia.


 Dar es Salaam.
Rais John Magufuli amewatunuku vyeti wajumbe wa kamati zilizofanya uchunguzi wa kiwango, aina na  thamani ya madini katika makinikia.
Vyeti hivyo alivyowatunuku leo Jumatatu Oktoba 23,2017 ni ishara ya kutambua uzalendo waliouonyesha wajumbe hao  walioteuliwa na Rais.
Wengine waliotunukiwa vyeti ni wajumbe waliohusika katika majadiliano kati ya Serikali na Kampuni ya Barrick Gold Corporation na kutia saini mkataba wa kutekeleza mwelekeo mpya wa namna kampuni hiyo itakavyoendesha biashara ya madini ya dhahabu yanayochimbwa katika migodi yake nchini.
Makubaliano mengine ni kulipa takriban Sh700 bilioni za kuonyesha nia njema ya kufidia madai ya upotevu wa mapato yaliyotokana na biashara hiyo.
Pamoja na hao, Rais Magufuli amemtunuku cheti Spika wa Bunge, Job Ndugai akiwa kiongozi wa muhimili wa Bunge ambao umetoa mchango katika ufuatiliaji wa rasilimali za madini nchini.
Spika Ndugai aliunda kamati mbili za kutathmini mfumo wa uchimbaji, usimamizi, umiliki na udhibiti wa madini ya Tanzanite na almasi.
@habari na mwananchi

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...