Monday, 23 October 2017

Wakazi wa kijiji cha Dirifu Mkoani Katavi wanalazimika kutumia maji machafu kutokana na uhaba wa maji kijijini hapo.


MPANDA

Wakazi wa kijiji cha Dirifu kilichopo manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wanalazimika kutumia maji machafu kutokana na uhaba wa maji kijijini hapo.
Baadhi ya wakazi kijijini hapo wameiambia Mpanda Radio kuwa tatizo la maji limekuwa sugu kwa muda mrefu katika kijiji chao hali inayowalazimu kunywa maji yanayotoka katika vyanzo visivyo salama.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji cha Dilifu Bwana Isamil Idd amekiri kuwepo kwa shida ya maji kaika kijiji hicho na kusema kuwa amelifikisha suala hilo katika ngazi husika kwa hatua zaidi za utatuzi
Kijiji cha Dilifu kina mwingiliano wa wakazi wengi wanaovutiwa na machimbo ya dhahabu kijijini hapo hali inayosababisha ubora wa huduma kutoendana na idadi ya wakazi wake.

SORCE:haruna Juma

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...