Wednesday, 2 August 2017

Wakazi wa Halmashauri ya manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wametakiwa kulipa kodi ya majengo ili kuepuka kulipa faini.



Alipozungumza na Mpanda Redio Afisa wa kodi za majengo mkoani Katavi Mashenene Benny amesema tunasubir muungozo ili kama  kutakuwa na utaratibu wa kupiga faini kwa wote ambao hawajalipa kodi za majengo,hivyo kutokana na mfumo ambao tutatumia unapiga faini wenyewe.

kuwa mwisho wa kulipa kodi ilikuwa ni mwezi wa saba na kwa sasa amewataka wananchi kujitokeza ili kulipia kabla ya faini kuanza kutumika kwa wote ambao hawajatimiza agizo hilo.

 Mashenene amesema bado wanaendelea kutengeneza bili za mwaka 2017/2018 na kuzitoa kwa wananchi ili waweze kujua kiasi wanachotakiwa kulipia .

Kwa upande wao baadhi ya wananchi wamelalamika kusema hawajaridhika na ulipaji wa kodi za majengo kutokana na kuwa na utofautiwa hadhi za majengo.

Pia wananchi wameiomba mamlaka ya Mapato kutoa elimu kuhusu ulipaji wa kodi za majengo hasa katika maeneo ya vijijini na kuangalia hadhi za nyumba.

Ni muda mrefu tangu mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) itangaze kuongezwa kwa muda wa ulipaji wa kodi za majengo.

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...