Wakazi wa kijiji cha Ikondamoyo katika halmashauri
ya Nsimbo mkoa wa Katavi wamelalamikia uwepo wa urasimu wa utoaji ajira katika mradi wa ujenzi wa barabara
unaoendelea katika eneo hilo.
Wakizungumza na Mpanda
Redio kwa nyakati tofauti wamesema tangu tarehe moja mwezi huu kutangazwa kwa
ajira mbali mbali , kumekuwa na utata
kutokana na wageni kutoka sehemu nyingine kuhodhi ajira za wazawa.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Ikondamoyo Bernad Yusuph amekiri kuwepo kwa tatizo hilo na kuahidi
kulifuatilia suala hilo kwa wakati ili kulipatia ufumbuzi wa kina.
Serikali ya Awamu ya Tano inasisitiza miradi yoyote ya maendeleo inayo fanywa maeneo mbali mbali
inchini kuhakikisha inawanufaisha wazawa wa eneo husika ili kuondokana na
tatizo la ukosefu wa ajira.
CHANZO:PAUL MATHIUS
No comments:
Post a Comment