Wananchi wa Halmashauri
ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wameipongeza serikali kwa kuanzisha kitengo
cha Dawati la jinsia linalosaidia
kutatua changamoto katika jamii husani maswala ya unyanyasaji.
Wakizungumza na Mpanda
Redio kwa nyakati tofauti tofauti wamesema kumekuwepo na msaada mkubwa kwa jamii na kuweza kutatua migogoro mbali mbali
hasa ya unyanyasaji wa kijinsia na ukatili katiak familia.
Kwa upande wake Afisa
wa kitengo cha dawati la jinsi katika jeshi la polisi katika
Halmashauri ya manispaa ya Mpanda
Hawa amesema kuwa wanazidi kutoa elimu kwa jamii kuhusu maana ya Dawati la
jinsia ili kupunguza vitendo vya kiukatili katika jamii.
Afisa huyo amesema
Takwimu ya mwaka 2017 ya ukatili katika jamii kwa watoto ulikua mkubwa
ukilinganishwa mwaka 2018 ambapo umeweza kupungua kwa kiasi kikubwa.
No comments:
Post a Comment