TABORA
Wananchi
wa kijiji cha makibo kata ya Nyahua wilayani sikonge mkoani Tabora
wamelalamikia ujenzi wa madaraja mabovu ya barabara za kijiji hicho
yaliyojengwa chini ya kiwango hali inayopelekea wao kuendelea kupata adha ya
usafiri.
Wakizungumza kijijini hapo baadhi ya wakazi hao wamesema madaraja hayo
yamejengwa bila weledi kwa sababu hayana vipimo maalumu na pia yamewekewa
udongo wa mfinyazi ambao baade utakuwa ni utelezi wakati wa mvua.
Akizungumza kwa njia ya simu Diwani
wa kata ya makibo bwana Shija Nkwema amekiri madaraja hayo kujengwa chini ya
kiwango na kwamba wapo katika hatu za kumrudisha mkandarasi aliyojenga madaraja
hayo kufanya ukarabati .
Hata hivyo Diwani wa kata ya Nyahua
amewataka wananchi wa kijiji hicho kuwa watulivu kwa sababu serikali ipo
kwa ajili ya kuwaletea wananchi maendeleo hivyo suala hilo litapatiwa ufumbuzi.
No comments:
Post a Comment