Ujenzi wa Zahanati ya kijiji cha Kajeje kata ya Kanoge Halmashauli ya Nsimbo unaoendelea utasaidia kutatua changamoto ya huduma za
afya katika kata hiyo.
Diwani wa kata ya Kanoge Salehe Mrisho akizungumza na Mpanda Radio
amesema huduma za afya zinaendelea kuboreshwa katika maeneo mabalimbali.
Amesema uboreshwaji huo
umeambatana na serikali kutoa gari la wagonjwa litakalohudumia wagonjwa
kuwafikisha Hosptali kwa wakati hasa akinamama wajawazito ambao wamekuwa
wakipoteza maisha kwa kuchelewa kufika hosptali.
Ujenzi wa Zahanati hiyo ya kijiji cha Kajeje umeingizwa kwenye bajeti ya mwaka wa fedha 2018/2019 ambapo
unatarajia kugharimu kiasi cha shilingi milioni 25.
Chanzo:Ester Baraka
No comments:
Post a Comment