MPANDA
Video Mwenyekiti wa Kijiji cha Stalike Christopher Anjero akizungumza na Mwandishi wetu Haruna Juma eneo la Tukio
Watu wawili wa familia moja katika kijiji cha Stalike Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi wamefariki dunia
kutokana na kula uyoga unaodhaniwa kuwa na Sumu na watatu wakiwa mahututi.
Mwenyekiti wa Kijiji hicho Christopher
Anjero ameelezea kisa hicho kuwa cha mara ya kwanza tangu miongo kadhaa
iliyopita ambapo amewataja marehemu hao kuwa ni
Frenki Mayaga na Erizabeth Joji.
Ndugu wa marehemu ambao wanamuuguza mama wa familia hiyo wameelezea
kusikitishwa na tukio hilo na kulitaja
kuwa maajabu.
Mpanda radio imemtafuta Mganga wa zamu wa hospitali ya Manispaa ya
Mpanda ili kujua taratibu za kitabibu zinazo endelea bila mafanikio kutokana na
kuto kuwepo katika eneo la kazi.
Chanzo:Alinanuswe Edward
No comments:
Post a Comment