NSIMBO
Mbunge wa Jimbo la Nsimbo mkoani Katavi Richard Mbogo amesema katika kipindi cha miaka miwili
iliyopita zaidi ya visima arobaini vimechimbwa katika jimbo hilo kwa ajili ya
kusaidia wananchi kupata maji safi na salama.
Richard Mbogo ameeleza baadhi ya mikakati ya ukamilishaji wa miradi ya
maji kwa mwaka wa fedha 2017/ 2018 akiitaja kuwa suluhu ya tatizo la maji
katika Vijiji vya kata ya Stalike na Itenka B, .
Katika hatua nyingine amesema katika mwaka wa fedha 2018/2019 maeneo
ya vijiji vipya yatafikishiwa miradi ya visima vya maji ili kuboresha huduma za
kijamii katika maeneo hayo.
Inaelezwa kuwa katika kipindi hicho cha miaka miwili upatikanaji wa
huduma ya maji safi na salama imepanda kutoka 34% mpaka 45%.
Chanzo :Alinnuswe
No comments:
Post a Comment