Serikali imeagiza utekelezaji wa Mradi wa Umeme Vijijini Awamu ya
Tatu (REA III) uanze mwezi huu wa Januari, 2018 sambamba na utekelezaji wa
Mradi wa Densification ambao upo kwenye utekelezaji.
Naibu Waziri Nishati, Subira Mgalu ametoa agizo hilo wakati wa
ziara yake ya kutembelea maeneo mbalimbali ambayo Mradi wa Umeme Vijijini
unatekelezwa Wilayani Kyela, Mkoani Mbeya.
Mgalu akizungumza na baadhi ya wananchi Wilayani humo ambao
wamemueleza kero mbalimbali zinazohusu masuala ya Nishati ya Umeme ambayo ni
kukatika kwa umeme mara kwa mara bila taarifa, kucheleweshwa kuunganishwa na
huduma ya umeme kwa ambao tayari wamelipia, baadhi ya Taasisi (shule, zahanati,
vituo vya afya na visima vya maji) kurukwa wakati wa utekelezaji wa Mradi wa
Umeme Vijijini Awamu ya Pili (REA II).
Baada ya kuzungumza na wananchi hao kwa nyakati tofauti, akijibu
kero zao, Naibu Waziri Mgalu aliagiza Mradi wa REA III uanze kutekelezwa ndani
ya Mwezi huu wa januari, 2018 bila kuchelewa.
No comments:
Post a Comment