Rais wa Tanzania Dkt. John PombeMagufuli |
Rais Magufuli ametoa agizo hilo muda mfupi baada ya Biteko kuapishwa leo Jumatatu Ikulu jijini Dar es Salaam na ameelezea kutoridhishwa kwake na namna viongozi na watendaji wa Wizara ya Madini wanavyotekeleza majukumu yao polepole na bila kujali maslahi ya nchi.
“Sheria hii imepitishwa na Bunge na mimi nikaisaini tangu mwezi wa saba mwaka 2017, mpaka leo ni miezi saba bado hamjasaini kanuni zake ili sheria ianze kutekelezwa, na wahusika wote wapo, yaani mpaka leo hamjaelewa Watanzania wanataka nini? Amehoji Rais Magufuli.
Kutokana na hali hiyo amemuagiza Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi kushirikiana na Naibu Mawaziri, Katibu Mkuu na Wakurugenzi wanaohusika katika Wizara ya Madini kuhakikisha kanuni hizo zinasainiwa.
Kamishna wa Madini Mhandisi Benjamin Mchwampaka na amemteua Profesa Shukrani Manya kuwa Kamishna wa Madini na pia kukaimu nafasi ya Mtendaji Mkuu wa Kamisheni ya Madini.
Kabla ya uteuzi huu Profesa Manya alikuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Idara ya Jiolojia.
Wakati huo huo, Rais Magufuli ameiagiza Wizara ya Kilimo kuhakikisha mbolea inafikishwa katika mikoa yote ya uzalishaji wa chakula ukiwemo Mkoa wa Rukwa ifikapo Ijumaa Januari 12, 2018.
Rais Magufuli amemuelekeza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kufuatilia jambo hilo na amebainisha kuwa endapo mbolea haitafikishwa katika maeneo hayo ifikapo Ijumaa wahusika waachie ngazi.
“Wakulima wanataka mbolea na muda ni huu, inasikitisha sana, fedha kwenye bajeti zimetengwa lakini mpaka leo mbolea haijawafikia wakulima, sasa mkoa kama Rukwa ndio tunaoutegemea kwa chakula, waziri yupo na watendaji wake wapo lakini mpaka leo mbolea haijapelekwa, wakulima watazalishaje chakula?
Rais Magufuli amewataka watendaji wote wa Serikali kutekeleza majukumu yao ipasavyo na ameonya kuwa hatosita kumfukuza kazi mtendaji yeyote atakayeshindwa kutekeleza wajibu wake kwa maslahi ya Watanzania.
“Nataka kila mmoja afanye kazi, Watanzania wanataka maendeleo, hakuna muda wa kubembelezana, kila mmoja afanyie kazi mambo yanayomhusu asisubiri kuambiwa, kule bandarini niliunda timu za kuchunguza madudu yaliyopo huko naambiwa kuna makontena 178 ya makinikia hayana mwenyewe, mengine yapo Ubungo, mengine bandari” ameongeza Rais Magufuli.
No comments:
Post a Comment