MBEYA
Jumla
ya Watu 456, wamepoteza maisha na wengine zaidi ya 700 wamejeruhiwa mkoani
Mbeya kutokana na matukio ya ajali za barabarani katika kipindi cha mwaka 2016
hadi 2017.
Akizungumza hali ya usalama ya mkoa
kwa mwaka 2017 mbele ya waandishi wa habari Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya,
Mohammed Mpinga amebainisha kuwa jumla ya makosa 82,211 ya ukiukwaji wa sheria
za barabarani yalipatikana katika kipindi cha mwaka 2017, wakati mwaka 2016
yalikuwa ni 66,172.
Kamanda Mpinga, amesema Mwaka jana
jumla ya watu 170 walipoteza maisha kutokana na ajali za barababani wakati
mwaka 2016, watu waliopoteza maisha ni 286 hivyo kuna upungufu wa asilimia 40.5
ya idadi ya vifo vilivyoripotiwa katika kipindi cha miaka miwili.
Kuhusu hali ya uharifu hali ya
uhalifu, kamanda Mpinga amesema jumla ya makosa 26,009 yameripotiwa kutokea
katika mkoa wa Mbeya kwa kipindi cha mwaka jana ikilinganishwa na matukio
32,943 yaliyoripotiwa katika kipindi kama hicho mwaka 2016.
Aidha Kamanda Mpinga amesema kwa
mwaka 2018 jeshi la polisi limeandaa mikakati mbalimbali ya kukabiliana na
wahalifu na uhalifu pamoja na kupunguza ajali za barabarani ikiwa ni pamoja na
kubaini muelekeo wa uhalifu na maeneo tete ili kuelekeza nguvu katika maeneo
hayo.
Chanzo:Eatv
No comments:
Post a Comment