Monday, 8 January 2018

Mvua iliyoanza kunyesha saa 11 asubuhi jijini Dar es Salaam imesababisha msongamano wa magari katika barabara mbalimbali za jiji hilo.


DAR ES SALAAM
Mvua iliyoanza kunyesha saa 11 asubuhi jijini Dar es Salaam imesababisha msongamano wa magari katika barabara mbalimbali za jiji hilo kutokana na maji kuingia barabarani.
Katika barabara ya Bagamoyo foleni ya magari ni kubwa huku eneo la Mbezi Massana kukiwa na maji yamejaa barabarani jambo linaloleta changamoto kwa wenye magari kupita eneo hilo.
Mbali na hiyo pia barabara ya Nyerere foleni nako ni kubwa kuelekea Tazara kutokana na mvua hizo.

Barabara ya Morogoro nako foleni ni hivyo hivyo kwa ukubwa wake kutokana na mvua kuendelea kunyesha.

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...