MPANDA
Idadi ya walio fariki kutokana na kula uyoga unaosadikiwa kuwa na sumu
katika kijiji cha Stalike wilaya ya Mpanda mkoani Katavi imeongezeka na kufikia
watu tatu.
Christopher Anjero ambaye ni Mwenyekiti
wa Kijiji hicho amezungumza na Mpanda radio kwa njia ya simu akieleza kuhusu
kifo cha Mariana Jerad Saanane ambaye ni Mama wa marehemu wawili walio fariki
siku ya jana.
Kisa hicho ambacho kimeiacha jamii ya eneo hilo katika
simanzi kinatajwa kuwa cha mara ya kwanza tangu miongo kadhaa iliyopita.
Frenki Mayaga amefariki
akipatiwa huduma ya kwanza katika kijiji cha Stalike huku Erizabeth Joji ambaye alikimbizwa hospitali
ya Manispaa ya Mpanda akiaga dunia mlangoni kwa daktari.
Mpanda radio imemtafuta Mganga wa zamu wa hospitali ya Manispaa ya
Mpanda ambaye amekana kueleza zaidi kuhusu suala hilo kwa madai ya kutokuwa
msemaji kwa sasa.
Chanzo:Alinanuswe Edward
No comments:
Post a Comment