TANGANYIKA
Wananchi wa Kitongoji cha Sijonga kata ya Kabungu wilayami Tanganyika
Mkoani Katavi wameulalamikia uongozi wa kijiji kwa kutokuwa na utaratibu wa
kutoa taarifa ya mapato na matumizi katika kijiji hicho.
Wakizungumza na Mpanda Radio kwa nyakati tofauti wananchi hao wamesema
katika kijiji hicho wamekuwa wakichangia michango mbalimbali kama ya maji
lakini wanashangazwa na kitendo cha kutosomewa mapato ma matumizi yaliyopo.
Kwa upande wake Afisa maendeleo ya jamii Kata ya kabungu na
ambaye ana kaimu nafasi mtendaji kijiji cha kabungu Othumani Kasamia ameshanganzwa na malalamiko
hayo na kusema kuwa wao kama viongozi taarifa za mapato na matumizi wanasoma
kila baada ya miezi mitatu na baada ya hapo wanabandika katika mbao za
matangazo ili kila mmoja aweze kujisomea.
Ni haki ya kila mwananchi kupewa taarifa za maendeleo katika eneo
analoishi hususani kujua mapato na matumizi.
Chanzo:Rebecca Kija
No comments:
Post a Comment