Wananchi wa Manispaa ya Mpanda ambao wanajihusisha na usajiriamali
katika vikundi mbalimbali wametoa maoni yao kuhusu mchango wa serikali katika
vikundi hivyo.
Agustina Kunikwiza ni mwenyekiti wa kikundi cha mwembeni ambacho
kinahudumiwa na serikali, amesema
serikali imewapatia kiwango cha fedha ambacho kikundi hicho wanatumia katika
shughuli za kilimo na ufugaji.
Aidha ametaja changamoto wanazokumbana nazo ikiwemo mtaji kutokana na wanakikundi kuongezeka hali
inayopelekea fedha hizo kutokutosheleza
na kuiomba serikali kuweza kuwaongezea fedha ili kuweza kuendeleza miradi yao.
Kila halmashauri hutenga asilimia 10 ya mapato yake kwaajili ya
kuwawezesha wanawake na vijana ili
kuweza kujikwamua kiuchumi na kuondokana na utegemezi.
Chanzo:Ezelina Yuda
No comments:
Post a Comment