MPANDA
Imeelezwa kuwa
kuendelea kuwepo kwa makundi ya watoto wengi kuishi katika hali hatarishi ni
kukithiri kwa matukio ya kikatili dhidi yao.
Kauli hiyo imebainishwa
na Baadhi ya Wakazi wa Misukumilo Mkoani Katavi ambapo wameeleza kuwa dhidi ya ukatili wa unaoendelea kufanywa kwa watoto hao
ndani ya jamii.
Wakizungumza na Mpanda
Redio Fm wakazi hao wamesema kuwa baadhi ya familia nyingi zimekuwa zikifanya
ukatili kwa watoto hasa ambao hawajwazaa na kushindwa kuwatimizia mahitaji
muhimu.
Wakazi hao wameongeza kuwa vitendo hivyo vya kikatili
vimepelekea watoto wengi kukimbia
makazi na kujiingiza katika makundi
mabovu.
Kumekuwa na wimbi kubwa
la watoto wa mitaani kutokana na vitendo
vingi vya kikatili ambavyo hutendewa hivyo kupelekea kushindwa kusoma na kuishia kutangatanga.
No comments:
Post a Comment