MPANDA
Tatizo la ukosefu wa choo linalokikabili kiwanda cha mbao kilichopo
misukumilo mjini Mpanda limetajwa kuendelea kutishia usalama wa wakaz wanaishi
jirani na kiwanda hicho.
Hali hiyo inakuja ikiwa ni siku mbili tangu mmliki
wa kiwanda hicho kuahidi ujenzi kuanza mara moja.
Mmoja ya wafanyakazi wa kiwanda hicho ambaye hakutaka kutaja
utambulisho wake ameiambia mpanda radio kuwa bado wanakumbana na adha hiyo
licha ya mmliki wake kuahidi ukarabati kuanza.
Nao wakazi ambao wanaoishi
kuzunguka kiwanda hicho wameomba mmiliki
wa kiwanda hicho kukamilisha haraka ujenzi wa choo ili kuepukusha magonjwa ya
kuambukiza.
sanjari na hayo taarifa zinarifu kuwa kiwanda hicho kilishawahi
kufungwa na serikali kutokana na kukiuka tarataibu kadhaa za kuanzishwa kwake.
No comments:
Post a Comment