MWANZA
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa
(Takukuru), Mkoa wa Mwanza imewaweka kiporo viongozi na makada wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM) baada ya kuahirisha kutoa taarifa ya uchunguzi dhidi yao
iliyopangwa kutolewa Januari 15.
Wanaochunguzwa kwa tuhuma za kujihusisha na
vitendo vya rushwa wakati wa mchakato wa uchaguzi ndani ya CCM ni pamoja na
katibu mwenezi wa CCM Wilaya ya Ukerewe, Nicholaus Munyoro; diwani wa Kata ya
Murutunguru, Musa Manka; diwani wa Kata ya Bukindo, Gabriel Gregory na Steven
Mazige ambaye ni mwenyekiti wa CCM Kata ya Ukerewe.
Makada hao walitiwa mbaroni na Takukuru Desemba
2, 2017 wakati wa mchakato wa uchaguzi wa viongozi wa CCM mkoani Mwanza
uliofanyika katika Uwanja wa CCM Kirumba kwa madai ya kukutwa wakigawana Sh400,
000 zilizosadikiwa kuwa rushwa iliyotolewa na mmoja wa wagombea.
Akizungumza kwa njia ya simu jana kuhusu suala
hilo, mkuu wa Takukuru Mkoa wa Mwanza, Ernest Makale amesema taasisi hiyo
itapanga siku nyingine ya kutoa taarifa ya uchunguzi dhidi ya viongozi hao
baada ya kushindwa kufanya hivyo Jumatatu iliyopita.
Chanzo:Paul Matius
No comments:
Post a Comment