MYANMAR
Kiasi ya Waislamu Warohingya 6,700 waliuwawa katika mwezi wa
kwanza wa ukandamizaji wa jeshi la Myanmar dhidi ya waasi katika jimbo la
Rakhine ambao ulianza mwishoni mwa mwezi Agosti.
Shirika la madaktari
wasio na mipaka MSF limesema idadi hiyo ni ya juu kabisa kwa makadirio kutokana
na ghasia zilizozuka tarehe 25 Agosti na kuzusha mzozo mkubwa wa wakimbizi.
Zaidi ya Warohingya 620,000 walikimbilia Bangladesh katika
muda wa miezi mitatu.
Ugunduzi wa kundi hilo unakuja kutokana na uchunguzi mara
sita wa zaidi ya watu 11,426 katika makambi ya Warohingya na ulifanyika katika
mwezi wa kwanza baada ya mzozo huo kuzuka.
SOURCE DW
No comments:
Post a Comment