KATAVI.
Wakazi wa mkoa wa
Katavi wametakiwa kuwa walinzi wa kutunza miundo mbinu ya umeme ili waweze
kupata huduma nzuri na kupunguza
kukatika kwa umeme mara kwa mara.
Yamebainishwa hayo na
meneja wa shirika la umeme (TANESCO) mkoa wa katavi mhandisi Julius Sabu wakati
akizungumza na mpanda redio ambapo amesema
wananchi wamekuwa wakichangia kuharibika kwa miundombinu hiyo.
Aidha amesema kuwa
shirika la umeme linafanya utaratibu wa kutenganisha laini za makazi ya watu na
maeneo ya viwandani ili kuondosha tatizo la kukatika kwa umeme unaotokana na
matatizo yanayosababishwa na viwanda kutumia laini moja na watumiaji wa kawaida.
Hata hivyo amewaomba
wananchi kujenga tabia ya kutoa taarifa pale wanapoona kuna shida ya umeme
katika maeneo yao ili kurahisisha kazi na kutatua changamoto kwa haraka.
CHANZO: REBECCA KIJA .
No comments:
Post a Comment