Wakazi wa kata ya Katumba Halmashauri ya
wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi wameilalamikia Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo
kwa madai kuwa halmashauri hiyo imewanyanga’anya gari la wagonjwa ambalo
limekuwa likitoa huduma kwa wagonjwa katika kata hiyo.
Malalamiko hayo yametolewa na wakazi hao
wakati wakizungumza na Mpanda Radio ambapo wamesema kuwa wamenyang’anywa gari
kwa madai kuwa wakazi wa Katumba hawana dereva wa kuendesha gari hilo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmshauri
hiyo Mh.Raphael Kalinga amekanusaha kuwanyang’anya gari la wagonjwa wakazi wa
Kata ya Katumba ambapo amesema lipo kwenye matengenezo baada ya kuharibika.
Aidha Kalinga amesema suala la
kuharibika kwa gari hilo limekwishatolewa ufafanuzi kuanzia kwa viongozi wa
Halmashauri,Mkoa hadi ngazi ya wizara.
Kata ya Katumba ina vijiji 16 na zaidi
ya wakazi elfu hamsini wanaotegemea huduma ya gari hilo.
Source: Issack
Gerald,
No comments:
Post a Comment