Halmashauri ya wilaya ya Mpanda mkoani
Katavi imekanusha kuhusu uwepo wa pembejeo feki zinazosambazwa na kutumika
katika msimu huu wa kilimo.
Hayo yamesemwa na afisa kilimo wa
halimashauri hiyo Bw. Fabian Kashindye alipokuwa akizungumza na mpanda radio
ambapo ameeleza kuwa kitisho hicho ni sawa na propaganda.
Zaidi ya asilimia 80 ya wananchi wa
Tanzania hutegemea kilimo katika kuendesha maisha na kipato cha kaya,wengi wao
ni kutoka vijijini ambao hukabiliwa na elimu duni kuhusu kilimo bora.
Hivi karibuni Waziri wa Kilimo,Dk Charles Tizeba ameitaja mikoa ya
Rukwa,Njombe,Iringa,Songwe na Mbeya kuongoza kwa kuuza mbegu feki za mahindi na
kusababisha madhara makubwa kwa wakulima, ikiwemo uzalishaji mdogo wa zao hilo
Source: Alinanuswe
No comments:
Post a Comment