NSIMBO
Wakazi wa kata ya
Itenka iliyopo halmashauri ya Nsimbo mkoani Katavi wameiomba serikali
kuwatengezea barabara ya Imilamate-Itenka hadi mjini Mpanda.
Kwa mujibu wa baadhi ya
wananchi hao wameiambia mpanda radio kuwa licha ya barabara hiyo kuwa kitovu
cha mawasiliano lakini imetelekezwa na serikali.
Wamsema wanahofia uhakika
wa barabara hiyo kupitika hasa katika musimu huu wa mvua kwani imekuwa
ikikatika na wao kubaki wako kisiwani.
Akijibu hoja za
wananchi hao mwenyekiti wa halmashauri ya Nsimbo Rafael Kalinga amesema tayari
halmashauri imeshawasilisha makadirio ya barabara zote kwa wakala wa barabara
vijijini na mijini (TARURA) wanachosubiri ni utekelezaji
Bwana Kalinga amewataka
wananchi kuwa wavumilivu wakati huu ambapo bado barabara hiyo ipo kwenye
mchakato wa matengenezo.
CHANZO: HARUNA JUMA .
No comments:
Post a Comment