Friday, 16 March 2018

Shule ya msingi inakabiliwa na uhaba wa vyumba vya madarasa na upungufu wa walimu.

Picha ya Jengo la shule


MLELE
Shule ya msingi Inyonga iliyopo katika halmashauri ya wilaya ya Mlele mkoani katavi inakabiliwa na uhaba wa vyumba vya madarasa na upungufu wa walimu.
Mkuu wa shule hiyo Mwalimu Neri Sokoni amesema kuwa shule hiyo ina idadi kubwa ya wanafunzi ambayo haiendani na vyumba vya madarasa hali inayosababisha wanafunzi zaidi ya 87 kusomea katika chumba kimoja cha darasa.
Aidha ameeleza kuwa licha ya shule hiyo kuwa na wanafunzi 1339 bado walimu waliopo hawakidhi mahitaji kwani mwalimu mmoja analazimika kufundisha zaidi ya wanafunzi 67.
Mwalimu Neri ameiomba serikali pamoja na taasisi mbalimbali na wananchi kusaidia kutatua changamoto hizo ili kuinua elimu katika shule hiyo.
Chanzo: Revocatus Msafiri

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...