Picha ya wananchi wa Mkoa wa Katavi |
KATAVI
Baadhi ya wakazi wa Mkoa wa
Katavi wamekuwa na maoni tofauti kuhusu ripoti ya Umoja wa Mataifa kuirodhesha
Tanzania kati ya nchi za mwisho kwenye orodha ya nchi ambazo watu wake wana
furaha duniani.
Mpanda radio imezungumza na
Bi Semeni Mwakatobe mkazi wa Majengo mjini Mpanda ambaye amesema kuwa moja ya
sababu za watu kukosa furaha nchini ni hali ya kiuchumi.
Hata hivyo mkazi mwingine wa
Mpanda Hotel mjini Mpanda bwana Jackson Juve
kwa upande wake amepingana na ripoti hiyo
Siku ya jana Umoja wa
Mataifa umetoa ripoti ya nchi zenye watu wenye furaha zaidi duniani na
kuiorodhesha nchi ya Tanzania katika nafasi ya 153 kati ya nchi 156 na kutaja
sababu ya nchi nyingi barani Afrika kushika nafasi za mwisho ni Magonjwa,
Viribatumbo, Madeni, migawanyiko/mipasuko ya kisisasa na msongo wa mawazo.
Katika ripoti hiyo nchi ya
Finland imeorodheshwa katika nafasi ya kwanza.
Chanzo: Haruna Juma
No comments:
Post a Comment