Friday, 16 March 2018

MWENYEKITI BAJAJI MANISPAA YA MPANDA AJIUZULU.



MPANDA.

Mwenyekiti wa Chama cha madreva pikipiki za tairi tatu maarufu bajaji halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi Bw.Rashid Rashid ametangaza kujiuzuru nafasi hiyo.
Katika taarifa yake ambayo ameitoa leo Bw.Rashid amesema, miongoni mwa sababu za kujiuzulu kwake ni pamoja na kukosa ushirikiano kutoka kwa madereva wenzake,ukosefu wa ushirikiano kwa kamati yake na kutotekelezwa kwa mipango mbalimbali wanayoipanga kama chama.

Aidha amesema changamoto iliyopo kwa sasa ni mgawanyiko wa wamiliki bajaji upande wa watumishi wa serikali kutozingatia kanuni na taratibu za umiliki wa chombo hicho cha usafiri pamoja na watu binafsi kulipishwa faini mara kwa mara bila utaratibu.

Mapema mwaka huu,baadhi ya madereva bajaji walikuwa wakilalamika kutozwa fedha mpaka elfu arobaini ili chombo chake cha usafiri kipewe namba ya usajili kwa ajili ya kuendesha shughuli zao wakiwa katika maegesho wanayopangiwa.

Chanzo: Issack Gerald

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...