Thursday, 15 March 2018

Viongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo wamelaani matukio mbalimbali ya uharifu yanayoendelea kujitokeza Mkoani Katavi.



KATAVI.

Viongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo Mkoani Katavi, wamelaani matukio mbalimbali ya uharifu yanayoendelea kujitokeza Mkoani Katavi na kusababisha mauaji ya raia na wengine kadhaa kujeruhiwa.

Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo John Malack pamoja na katibu wa chama hicho Bw.Joseph Mona wakizungumza na Mpanda Radio,wamevishauri vyombo vyote vya ulinzi na usalama kutafuta namna ya kudhibiti waharifu ili kuimarisha usalama wa raia ma mali zao.

Kwa upande wao baadhi ya vijana Mkoani Katavi wamesema, ukosefu wa ajira kwa vijana wengi waliopo mitaani ni miongoni mwa vyanzo vinavyochangia kuongezeka kwa uharifu.

Kuanzia mwezi Januari mpaka Machi mwaka huu,zaidi ya watu watatu wamefariki dunia katika matukio matatu tofauti yakiwemo matukio mawili ya ujambazi Januari 27 kata ya Ugalla,Februari 25 mwaka huu katika Mgodi wa dhahabu wa Isulamilomo wilayani Mpanda na tukio jingine la Januari 22 likihusisha kifo cha mwanafunzi aliyeuwawa kikatiri wilayani Tanganyika.

Chanzo:Issack Gerald

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...