Thursday, 15 March 2018

Mkuu wa wilaya ya Tanganyika amesema wilaya hiyo imeshapeleka mapendekezo kwa ngazi zote ili kubadili jina la Hamlashauri ya wilaya hiyo.

Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Salehe Mbwana Mhando


TANGANYIKA
Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Salehe Mbwana Mhando amesema wilaya hiyo imeshapeleka mapendekezo kwa ngazi zote ili kubadili jina la Hamlashauri ya wilaya hiyo kutoka halmashauiri ya wilaya ya Mpanda
Akizungumza na Mpanda radio mapema leo Mhando amesema kikao cha ushauri cha wilaya hiyo (DCC) kimeshawasilisha mapendekezo hayo katika kikao cha ushauri cha mkoa (RCC) na kasha TAMISEMI na sasa wanasubiri utekelezaji.
Muhando ameongeza kuwa halmashauri ya wilaya ya Mpanda kuwa katika wilaya ya Tanganyika imekuwa ikileta mkanganyiko kwa watu wengi kiasi cha kushindwa kutofautishwa na halmashauri ya Manispaa ya Mpanda
Wilaya ya Tanganyika imetokana na wilaya ya Mpanda iliyokuwa na Halmashauri mbili hapo kabla
Chanzo:Restuta Nyondo

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...