MAAMBUKIZI
ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) nchini yamezidi kupungua kutoka wastani wa asilimia
5.1 mwaka 2011/2012 hadi kufikia wastani wa asilimia 4.7 kwa mwaka 2016/2017.
Hayo
yamebainishwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan wakati akizindua takwimu
hizo mpya za viashiria na kukithiri kwa Ukimwi kwa utafiti wa mwaka 2016/2017
wanawake ni asilimia 6.5 na wanaume 3.5.
Aidha
amesema inakadiriwa Watanzania milioni 1.4 wanaishi na VVU huku kwa vijana wa
umri wa miaka kati ya 15 na 24 ni asilimia 1.4 ambapo kati ya asilimia hiyo
wanaume ni asilimia 0.6 na wanawake ni asilimia 2.1.
Katika
Takwimu hiyo mpya,Mkoa wa Katavi umeendelea kuwa na asilimia 5.9,Rukwa
asilimia 6.2 huku Mkoa wa Njombe ukiongoza kwa asilimia 11.4 ya maambukizi ya
Ukimwi.
Source: Issack
Gerald,
No comments:
Post a Comment