Saturday, 2 December 2017

Mbunge wa Jimbo la arumeru Mashariki Joshua Nassari, amevamiwa na watu wasiojulikana nyumbani kwake Usa River mkoani Arusha




Mbunge wa Jimbo la arumeru Mashariki Joshua Nassari, amevamiwa na watu wasiojulikana nyumbani kwake Usa River mkoani Arusha na kunusurika kupigwa na risasi ambazo zimeua mbwa wake.
Katika ukurasa wake wa twitter,Nassari ameandika ujumbe akitoa taarifa kuwa watu hao wamevamia nyumbani kwake usiku wakiwa na silaha za moto ambazo wamewafyatulia mbwa wake.

Mbunge huyo mara kadhaa amekuwa akiripoti katika mitandao ya kijamii kuwa amekuwa atishiwa kuuawa mara kwa mara.
Hakuna kauli ya jeshi la polisi ambayo imetolewa kuzungumzia tukio hilo.
Source: eatv,

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...