Chama cha Mapinduzi CCM kimeweka wazi sababu iliyowafanya wakatae
kumpokea msanii Wema Sepetu kwenye chama hicho, ambaye hapo jana ametangaza
kurudi kundini.
Akizungumza
na mwandishi wa East Africa Television, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM
Humphrey Polepole, kwanza amekanusha kumpokea mwanachama huyo na kusema kwamba,
hakufuata utaratibu sahihi kuweza kurejea kwenye chama hicho ambacho alikiasi.
Pole
Pole ameendelea kwa kusema kwamba CCM inajidhatiti katika kujijengea misingi
imara na wanachama wake, hivyo wanataka mtu ambaye anaenda CCM awe
amejidhatiti, kwani hawataki kuja kubeba mizigo ya lawama.
Pamoja
na hayo Polepole amekanusha taarifa zilizosambaa mitandaoni kwamba msanii huyo
ameshawishiwa kurudi CCM baada ya kuahidiwa atasaidiwa kumaliza kesi yake
inayomkabili mahakamamni, pamoja na kunusuru kubomolewa kwa nyumba yao.
No comments:
Post a Comment