Waislam nchini Misri leo wamefanya sala katika msikiti ulioko
kwenye rasi ya Sinai ulioshambuliwa wiki iliyopita ambapo watu 305 waliuawa.
Televisheni ya serikali imeonesha waumini wakiwa ndani ya
msikiti huo wa al-Rawdah kwenye eneo hilo la kaskazini nchini humo lililo
katika hali tete katika kile kilichoelezwa na televisheni hiyo kuwa ilikuwa ni
ishara ya kuonesha mshikamano na familia za wahanga wa shambulizi hilo pamoja
na kupinga ugaidi.
Maombi hayo yameongozwa na Sheikh Ahmed al-Tayeb kiongozi wa
mafundisho ya waislamu wa madhehebu ya kisuni.
Katika mawaidha yake wakati wa maombi hayo al-Tayeb amesema
washambuliaji hao ni waovu wanaostahili kuuawa.
Hadi sasa hakuna kundi lililodai kuhusika na shambulizi hilo
ambalo ni baya zaidi katika historia ya Misri.
No comments:
Post a Comment