MPANDA
Baadhi ya wakazi wa Kata ya Katumba
Halmshauri ya Wilaya ya Nsimbo mkoani Katavi,wamewalalamikia baadhi ya wauguzi
na madaktari wa kituo cha afya cha Katumba ikiwemo Zahanati ya Kaminula kutumia
lugha chafu kwa wagonjwa.
Wakazi hao ambao hawakutaka kutaja
majina yao wakihofia usalama na kunyimwa matibabu katika kituo hicho wamesema
tatizo la baadhi ya wagonjwa kunyanyaswa lipo kwa muda mrefu.
Aidha baadhi ya wakazi wa Katumba
wamelalamika kufukuzwa na kunyimwa matibabu wanapohoji tatizo la kutokuwepo kwa
umeme katika katika kituo hicho licha yaShirika la wakimbizi duniani UNHCR na
Kanisa la FPCT limeshiriki kutoa Sola na
betri katika kwaajiri ya umeme.
Kwa upande wake Mkuu wa kituo cha
afya cha Katumba Dkt. Gabriel Ngonyani amekataa kuzungumza na Mpanda Radio kuhusiana na malalamiko hayo kwa madai
kuwa mpaka apate kibali cha mwajiri wake.
No comments:
Post a Comment