Wednesday, 13 September 2017

Baadhi ya wafanyabiashara katika soko la mpanda hotel wameiomba serikali kuwatafutia maeneo kwa ajili ya kufanyia biashara baada ya kuondolewa sokoni hapo.



MPANDA.
Baadhi ya wafanyabiashara katika soko la mpanda hotel Mkoani Katavi wameiomba serikali kuwatafutia maeneo Mbadala  kwa ajili ya kufanyia biashara baada ya kuondolewa katika eneo lao la biashara sokoni hapo.

Wakizungumza na mpanda redio baadhi ya wafanyabiashara hao  wamesema kwa sasa wameondolewa katika eneo hilo kwa kinachosemwa wapo karibu na kituo cha Afya Town Clinic   na hawajui wapi watafanyia biashara zao.  

Hata hivyo wafanyabiashara wamesema ushuru wanatoa kama inavyopaswa ila wanashangaa kwanini viongozi wanashindwa kushughulikia malalamiko yao ya kukosa eneo la kudumu la kufanyia biashara zao.


Kwa upande wao viongozi wa soko hilo wameshindwa kutoa ushirikiano juu ya malalamiko ya  wafanyabiashara hao.

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...