DAR ES SALAAM.
Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Anga (TCAA) imeingia
makubaliano na kampuni inayojihusisha
na mifumo ya anga kutoka nchini Ufaransa ya Thales kununua rada mpya nne.
Tukio hilo limeshuhudiwa na Waziri wa Ujenzi uchukuzi na
mawasiliano Profesa Makame Mbarawa na
wadau wengine wa usafiri wa anga nchini.
Upande wa Serikali mkataba umesainiwa na Mkurugenzi wa Mkuu
wa TCAA Hamza Johari na upande wa Thales amekuwa ni Meneja wa masoko wa kanda
kutoka kampuni ya Thales Abel Aberr Carr.
Mkurugenzi wa Mkuu wa TCAA Hamza Johari amesema kwa sasa
Tanzania ina rada moja pekee na uwezo wake kiufanisi umepungua kutokana na
mabadiliko yanayotokea kwa haraka katika sekta hiyo, sanjari na kuongezeka kwa
ndege zinazotumia anga la nchi.
Kwa upande wake Profesa Mbarawa amesema kufungwa kwa rada
hizo kutaongeza imani ya wadau wa sekta ya usafiri wa anga dunia kuwa na imani
na kutumia anga la Tanzania, hivyo watalii wataongezeka kwakuwa wanajua usafiri
wa anga nchini kwetu ni wa usalama.
No comments:
Post a Comment