Mh. Julius M. Kaondo |
RUKWA.
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa
Julius M. Kaondo amewapiga marufuku walimu wa shule za msingi na sekondari kuacha
tabia ya kuwafanyisha kazi ngumu na kwenye jua kali wanafunzi wenye ulemavu wa
ngozi albino kwani wanawahatarisha afya zao na kupelekea kupata saratani ya
ngozi.
Akizungumza jana wakati akizindua kituo maalumu cha upimaji
wa kielimu (Nkomolo Assessment Centre) Kilichopo Katika eneo la shule ya msingi
Nkomolo wilayani humo mkurugenzi huyo alisema kuwa kitendo hicho kinahatarisha
afya za wanafunzi hao na hivyo kuwaweka Katika mazingira ambayo yanaweza
kufupisha maisha yao.
Amesema kuwa watu wenye matatizo ya ualbino hawapaswi kukaa
Katika mionzi mikali ya jua kwani Inawasababishi ngozi zao kupata saratani
hivyo ni busara kuwachukulia kuwa ni watu maalumu na wanahitaji uangalizi
maalumu ilikuwakinga na maradhi ambayo yanaweza kuwadhuru.
Aidha amewasisitiza wanafunzi wote wenye ualbino kutumia
mafuta yao maalumu wanayopewa kama msaada ama kuyanunua ili kuzuia mionzi ya
jua kwani baadhi yao wamekuwa hawayatumii kwakukosa elimu sahihi na hivyo
kujikuta wakisumbuliwa na matatizo ya ngozi.
No comments:
Post a Comment