Mechi ya kwanza ambayo nilikuwa kati ya SUPERBOYS vs MIGAZINI mechi iliyochezwa majira ya saa 8 mchana ambayo iliisha kwa migazini kuondoka kifua mbele kwa kuwafunga super boy goli 1 kwa bila ambalo goli la pekee la migazin fc lilifungwa na Emanuel Iguluta katika kipindi cha kwanza na kuwapa migazinifc kutinga hatua ya robo finali ambalo mgazini fc watapambana na mshindi wa leo kati ya KASHATOvsILEMBOFC katika nusu final itakayochezwa siku ya tarehe 7 Mwezi huu katika majira ya SAA 10 jioni.
Picha ya juu ni wachezaji wa timu ya nyererefc
Picha hii wachezaji wa timu ya kotazifc
Pia robo fainali ya pili iliyochezwa muda wa saa10 jioni kati ya NYERERE FC KOTAZI FC mechi hii nilikuwa piga nikupige baada wachezaji wa timu zote mbili kuzawadiwa kadi nyekundu moja upande wa nyererefc na nyingine upande wa kotazifc na matokeo ya dakika 90 kuisha na matokeo yalikuwa goli 1 kwa 1 kati ya nyererefc na kotazifc na kukubaliana kupiga penati na nyerere ndio waliofungua dimba la kupiga penati baada kupiga penati kotazifc kuondoka na ushindi wa penati 4 kwa 3 Mara baada ya nyererefc kukosa penati mbili mechi hiyo ya robo fainali ya pili iliisha kwa kotazifc kuondoka kifua mbele na kushubiri mshindi wa mechi ya kwanza ya mashindi wa robo fainal ambayo itachezwa leo kati ya BOKO FC vs MAGOROFANI FC na nusu fainal ya kwanza itakayochezwa mapema Leo tarehe 05 mwezi 7 majira ya saa 8 mchana.
Picha ya juu ni kocha wa timu ya nyererefc na mwandishi wetu
Mechi za robo fainali za Leo ni kati ya BOKO FC vs MAGOROFANI FC mechi hii itachezwa mapema mida ya saa 8 mchana na Mshindi atacheza na KOTAZIFC siku ya tarehe 07 mwezi huu mida ya saa 8 mchana na mechi ya pili ya ya mchezo wa robo fainali itakayochezwa majira ya saa10 jioni itakuwa katika ya KASHATOvsILEMBOFC na mshindi atakutana na MIGAZIN FC katika hatua ya nusu fainali ya pili itakayochezwa majira ya saa 10 jioni.
Hatua ya fainali la kombe la mashindano ya sports update super cup kilele chake kitakuwa siku ya jumapili ya tarehe 09 mwezi huu.
katika mashindano ya sports update super cup mshindi wa kwanza atapata kikombe ,jezi pea moja na mpira,
mshindi wa pili atapata jezi pea moja na mpira na mshindi wa tatu atapata jezi pea moja.
No comments:
Post a Comment