KATAVI
Mashehe watano akiwemo Mwenyekiti wa Halmashauri
ya Baraza Kuu la Waislamu (Bakwata) Mkoa wa Katavi, Shehe Shaaban Bakari
wamesema kujizulu kwao ni kutokana na shehe wa Mkoa wa Katavi kukiuka Katiba ya
Bakwata.
Baadhi ya wajumbe waliojiuzulu wakizungumza na Mpanda Radio,wamemtuhumu Shehe wa Mkoa Ally Hussein kuwa kinara wa kukiuka katiba ya Bakwata.
Wajumbe wengine wa baraza la mashehe Mkoa
waliojiuzuru ujumbe ni Shehe Mashaka Nassoro Kakulukulu na Hassan Mbaruku.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya
Bakwata Mkoani Katavi Shehe Shaban Bakari ambaye naye amejiuzuru nafasi hiyo,amesema
Shehe wa Mkoa wa Katavi Ally Hussein amekuwa akizuia maendeleo ya dini ya
kiislamu kwa kutokubaliana na maamuzi ya vikao halali.
Hata hivyo Shehe wa Mkoa wa Katavi Ally Hussein
amekana tuhuma dhidi yake akisema ni fitina zinazofanywa na waliojiuzuru na wanatarajia
kufanya kikao ili kutoa maazimio kutokana na hali iliyotokea.
SOURCE: Alinanuswe
Edward.
No comments:
Post a Comment