Wataalamu kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba
na Maendeleo ya Makazi wakitoa elimu jinsi ya kutumia mfumo wa Government electronic Payment Gateway
kwa watendaji wa Halmashauri ya Kinondoni.
Watendaji wa Baraza la Ardhi na Nyumba
la Wilaya ya Kinondoni wakipewa mafunzo jinsi mfumo mpya wa ukusanyaji maduhuli
ya Serikali utakavyokuwa unatumika.
Elimu ya jinsi ya kutumia mfumo mpya wa
kielektroniki ikitolewa kwa watendaji wa manipaa ya Temeke jijini Dar es
Salaam.
DAR ES SALAAM,
Wizara ya Ardhi, Nyumba
na Maendeleo ya Makazi imeanza rasmi kutumia mfumo wa kielektroniki wa Government
electronic Payment Gateway (GePG)
katika makusanyo ya kodi ya pango la ardhi pamoja na tozo nyingine zinazotokana
na sekta ya ardhi nchini.
Mfumo huu
utamrahisishia mwananchi kulipa kodi ya pango la ardhi popote alipo, ikiwa ni
pamoja na kulipia tozo nyingine mbalimbali za sekta ya ardhi. Pia mfumo wa GePG,
utamuwezesha mwananchi au mmiliki wa kipande cha ardhi, kujua anadaiwa kiasi
gani cha kodi ya pango la ardhi na kulipia popote alipo bila kusumbuka kufuata
huduma hizo katika vituo vya makusanyo.
Majaribio ya ukusanyaji
kodi ya pango la ardhi kwa kutumia mfumo wa kielektroniki yalifanywa katika
mikoa ya Dar es Salaam na Pwani, baada ya mafanikio makubwa kuonekana elimu
ikatolewa kwa watendaji wote wa sekta ya ardhi katika Halmashauri zote za mkoa
wa Dar es salaam kabla ya zoezi hilo kuhamishiwa mikoani.
Mwananchi yeyote
anayemiliki kiwanja au shamba lililopimwa na kuwa na hati, ataweza kutumia simu
yake ya mkononi kujua kiasi cha kodi ya pango la ardhi anachodaiwa na kukulipa
kwa kutumia simu yake ya mkononi pia.
Kwa zile huduma
nyingine za sekta ya ardhi ambazo zinahusisha malipo kama vile upekuzi katika
daftari la msajili (official serach),
mwananchi atapaswa kutembelea ofisi za Wizara ya ardhi zilizo katika eneo lake
na kupatiwa makadirio ya kulipia huduma husika pamoja na namba ya malipo itakayomuwezesha
kulipia aidha kwa njia ya benki au simu ya mkononi.
Kwa sasa kikosi kazi
kinachotoa mafunzo juu ya matumizi ya mfumo huu kimeshaanza kuelemisha mikoa
mingine baada ya kupata mafanikio mazuri katika mkoa wa Dar es Salaam. Lengo kubwa
la kutumia mfumo huu ni kuongeza ufanisi katilka ukusanyaji wa maduhuli ya
serikali pamoja na kurahisisha ulipaji kodi ya pango la ardhi nchini,
No comments:
Post a Comment