waziri wa mambo ya ndani Mh.Mwigulu Nchemba |
Waziri wa mambo ya ndani Mh. Mwigulu Nchemba ametishia
kuwafutia uraia watanzania wapya wa Katumba mkoani Katavi ambao wamekuwa
wakimbizi kwa muda mrefu kutokana na tabia ya
baadhi yakubaguana kitaifa na kikanda.
Waziri Nchemba amesema hayo jana wakati
alipopita kwenye kambi kuangalia usajili unaendeleaje ambapo
amesema wananchi hao waliopewa uraia wakitokea burundi wakati
wa vita ya kikabila miaka 1972 wamekuwa na tabia ya ubaguzi hata kufikia
kushindwa kusaidiana kwenye biashara zao.
Waziri amewaambia wananchi hao kuwa yeyote atakayeleta mambo
ya ubaguzi ikiwa ni pamoja na kubaguana kibiashara katika jamii hatosita kumfutia uraia
alioupata kwani Watanzania hawana mambo ya kibaguzi.
Pamoja na hayo Kiongozi huyo ametumia muda huo kuwataka
Watanzania kuwa na utanzania ndani ya mioyo yao na waache tabia ya kutaka
kukwamisha kila kitu kinachofanywa na serikali kwa kuweka vikwazo mbele ili
vitu visifanikiwe.
No comments:
Post a Comment