MPANDA
Wakazi wa kijiji cha Kamakuka kilichopo kata ya Kakese wameitaka serikali kuchukua hatua dhidi ya Mkandarasi aliye shindwa kukamilisha Ujenzi wa
dalaja linaunganisha kijiji hicho na kijiji cha Kampuni .
Wameiambia Mpanda radio kuwa uongozi wa kijiji na Kata umeshindwa kutatua
kero hiyo ambapo wananchi hulazimika kupita majini hali ambayo ni hatari.
Mmoja wa viongozi ambaye ni mwenyekiti wa kitongoji
cha Ipwaga Bw Moses Taratibu amesema kunahujuma katika utekelezaji wa mradi huo
ambapo hata hivyo ameshindwa kumtaja mkandarasi aliye husika.
Licha ya eneo hilo kuwa maarufu kwa uzalishaji wa
Mpunga na mahindi
suala la miundo mbinu ya barabara ni kikwazo kwa mstakabari wa maendeleo ya
wakazi wa eneo hilo.
Chanzo:Alinanuswe Edward
No comments:
Post a Comment