Tuesday, 12 September 2017

Benjamin Netanyahu amewasili nchini Argentina kwa ziara ya siku mbili akilenga kuimarisha mahusiano na taifa hilo.

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu

YERUSALEMU 
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amewasili nchini Argentina kwa ziara ya siku mbili akilenga kuimarisha mahusiano na taifa hilo lililo na idadi kubwa ya Wayahudi Amerika Kusini.

Ziara hiyo ni ya kwanza kuwahi kufanywa na waziri mkuu wa Israel tangu kuundwa kwa taifa la Israel mwaka 1948.

Netanyahu atazitembelea pia Colombia na Mexico kabla kuelekea New York, ambako atalihutubia baraza kuu la Umoja wa Mataifa tarehe 26 mwezi huu.

 Pia atakutana na rais Mauricio Macri na anatarajiwa kumshinikiza atoe maelezo kuhusu mashambulizi mawili ya kigaidi Argentina ambayo mpaka sasa bado ni kitendawili.

Israel na Argentina zimeituhumu Iran kwa kuhusika na mashambulizi ya mabomu mjini Buenos Aires miaka ya 1990 ambapo watu 29 wameuawa katika ubalozi wa Israel na wengine 85 kuuliwa katika kituo cha kiyahudi. 

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...